wasomaji wangu wa blog habari zenu, leo nilikua nataka kushare na nyinyi one thing. kuna relation zingine ni ngumu mno kumuelewa mwenzako anataka nini na kama kweli anakupenda. kuna watu wengine hawajiweki wazi kwa wapenzi wao wapo na kama swala la pesa anaprovide , kwenye sex kawaida lakini kwenye kushow up love yuko mbali, hataki umtembelee, hataki uwajue marafiki zake kama mwanaume basi marafiki zake wa kikeau mwanamke basi wakiume tena ukimgusia hilo unaambiwa usimfuatilie
pia ugumu mwingine nikuwa hataki kuacha urafiki na watu ambao wewe mpenzi wake hauwataki. kikubwa wewe kama mpenzi wake hataki ushike simu yake, je kama mtu yupo safi na anajiamini na anayoyafanya kwa nini akataze simu. mpenzi huyu anataka mwenziwe amfikiriaje.sisemi watu mchunguzane kwenye simu zenu ila ni uhuru flani ambao hata ukiambiwa naomba simu yako unatoa.
Na hali hii ni tofauti na mlivyo anza uhusihano na yeye. naomba munisaidie kwa hili